Sala ya jubilei

Sala kwa ajili ya Jubilei ya miaka 25 tangu

ilipoanza Misioni yetu ya Tanzania

 

Ee, Mungu, Bwana na Baba yetu tunakushukuru kwa kazi ya mikono yako,
kila kitu tunachokiona  ni tuzo  kutoka kwako, zawadi ya Maongozi yako.
Tunakushukuru kwa ajili ya wale wote ambao wameshiriki katika ukuaji wa Misioni hii.
Kila siku Wewe umetutangulia katika kila kazi na kwa upendo wako umefanya Misioni yetu iwe bustani nzuri sana, machoni pa watu wengi.
Sisi sote tunakushukuru!
Yote uliyotuahidi  umeyatimiza kwa nguvu ya uwepo wako,  na ya Upendo wako wa kibaba.
Sisi sote tunakushukuru!
Uangalizi wako wa Baba mwenye upendo umeimarisha nguvu zetu na  ari yetu ya kukutumikia
Sisi sote tunakushukuru!
Wewe unaendelea kuiangalia na kuitegemeza kwa njia ya Roho wako Misioni yetu kwa sababu  uliijenga  kwa ajili yako  mwenyewe  kama sehemu  ya baraka
Sisi sote tunakushukuru!
Bwana,  kila kitu ni zawadi yako,  hatuna chochote cha kukurudishia  isipokuwa makosa yetu na udhaifu wetu. Tunakuomba msamaha Bwana,  kwa sababu hatujakurudishia chochote kinacholingana na upendo wako mkubwa na neema zako nyingi. Ee Bwana usiiache kazi ya mikono yako! Endelea kulibariki Shirika letu na Misioni yetu kwa kutupatia miito mingi na mitakatifu  na pia endelea  kutusaidia  kutimiza kwa uaminifu ahadi  tulizokuwekea. Tunakuomba si kwa mastahili yetu, kwa sababu hatustahili, bali kwa mastahili ya Kristo Yesu Mwanao. Kwa maombezi ya Bikira Maria Bibi wa  Misioni  yetu, ya Mtakatifu Yosepu mhasibu wetu, mt. Ursula, fanya ili  sisi sote tuisikie  leo nguvu ya enzi yako, ya utukufu wako juu ya Misioni yetu na juu ya kila   mursula  wa Tanzania. AMINA