Maisha

MTAKATIFU  URSULA  LEDOCHOWSKA

Mwanzilishi  wa  Shirika la Wa-Ursula

wa Moyo  wa Yesu Mteswa

 

 

Julia Ledochòwska alizaliwa mwaka 1865 huko Austria.  Baba yake Antoni Ledòchowski alikuwa mzaliwa wa Poland. Mama yake Josefina Salis Zizer alikuwa mkaaji  wa Switzland. Dada yake mkubwa Maria Theresia Mwanzilishi wa Wamisionari wa Mt. Petro Klaver na  Mdogo wake  Vladimiro alikuwa Mkuu wa Wajesuiti,  kwa miaka mingi.

Maisha_3

Alipokuwa na miaka 21 Julia aliingia Shirikani katika Konventi ya Wa-Ursula wa Kracow. Aliweka nadhiri zake mwaka 1889 na kupata jina la kitawa URSULA.Kuanzia siku hiyo, na kwa zaidi ya miaka kumi, alijitolea kwa bidii kubwa  kwa kufundisha na kuelimisha. Mwaka 1904 Mama Ursula aliteuliwa kuwa Mama Mkuu wa Konventi ya Krakovia. Akifanya  kazi hii alipata nafasi ya kutekeleza uanzishaji wa kazi za kitume zenye ujasiri  kwa wakati ule. Kwa mara ya kwanza huko Poland alianzisha Hosteli kwa ajili ya wasichana wa Chuo Kikuu, alianzisha pia Chama cha Bikira Maria, na mafunzo mbalimbali juu ya dhana za dunia. Mwaka 1907, kwa baraka ya Baba Mtakatifu Pio wa kumi, Mama Ursula alianzisha misheni mpya huko Urusi,  katika mji wa Petersburg, Makao Makuu ya ufalme wa Kirusi.

Mwaka  1914 ilianza vita ya kwanza ya dunia. Mama  Ursula, kama raia wa Austria, alipaswa kuondoka haraka  Urusi na  kuelekea Sweden, kwa kuwa karibu zaidi na jumuiya yake.Maisha_2 Huko  Sweden,  ingawa alijisikia mpweke, alijitahidi kuwasiliana na watu wa mahalia na baada ya muda aliwashawishi masista wake ili waende huko Sweden na Denmark. Huko alifanya kazi mbalimbali kwa kuwasaidia watu, tena kwa bidii na bila kuchoka alijitahidi  kutetea usawa na heshina ya mwanadamu. Alikuwa na kipaji maalum kilichomfanya aweze kuwaunganisha watu wa fikra na  madhehebu mbali mbali katika lengo moja; kwa mfano kwa njia ya mikutano na semina, kupata msaada kwa kuwasaidia majeruhi wa vita vya kwanza vya dunia.

Alifungua chuo cha lugha kwa wasichana wa Scandinavia huko Sweden… na baadaye huko Denmark, alianzisha Chuo cha Home Craft  na Nyumba kwa ajili ya watoto yatima. Alirudi Poland  mwaka 1920 na kwa ruhusa ya Makao Makuu ya Baba Mtakatifu, huko Pniewy, aliunda tawi jipya la Wa-Ursula: Shirika la kipapa la Masista Wa-Ursula wa Moyo Mtakatifu  wa Yesu Mteswa.

Maisha_5

 

Yeye alichukua yale ya muhimu katika maisha na karama za Shirika la Wa-Ursula wa zamani na alibadilisha mengine kwa kulingana  na mahitaji ya utume ya shirika jipya katika ulimwengu wa wakati wake. Lengo la kwanza la Shirika jipya lilikuwa  kuwasaidia watoto na vijana wenye kuhitaji msaada, tena kuwa tayari kwa mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya kila nchi na kila mazingira.

Dhima  ya pekee ya Shirika ndani ya Kanisa ni kumtangaza Kristu, Upendo wa Moyo wake, kwa njia ya malezi na elimu ya watoto na vijana, huduma kwa ndugu walio wahitaji sana na wanaodhulumiwa na pia kwa njia ya kazi  nyingine katika uwanja wa mahubiri ya Injili kwa ulimwengu.”( Kat. No. 4)

Huko Pniewy – Poland  alianzisha chuo cha Home Craft,   alipanga semina mbalimbali kwa ajili ya makatekista, alianzisha Chama cha Ekaristi kwa vijana na  alifungua nyumba mbalimbali kwa ajili ya watoto yatima.

 

Maisha_4

 

 

Alijitoa sana  kwa ajili ya waliohitaji zaidi.

 

Shirika limeenea kwa muda mfupi  katika nchi ya Poland na baadaye  Italia (1928) na Ufaransa (1930). Mama Ursula Ledòchowska ametoa fundisho moja la matumaini duniani, kwamba mambo yote yatakuwa mazuri tukimtanguliza Kristu. Kwa uwezo wake pamoja na  njia yake ya kuwatumikia na kuwafariji watu kwa furaha, katika shida zao mbalimbali,  Mama Ursula daima alikuwa mfano wa furaha na  wa mtu mwenye kukubali mapenzi ya Mungu.

Utakatifu kwa Mama Ursula ni: Kufanya matendo madogo na rahisi kwa upendo wa pekee…

Kwa hiyo leo yeye anatukumbusha sisi sote kwamba utakatifu ni kwa ajili ya wote na  siyo kwa mapadre na masista tu. Wote tunaweza kuwa na  tumaini kwamba kwa maisha ya kawaida tunaweza kuufikia utakatifu tukifanya yote vizuri na kwa upendo.

Mama Ursula aliaga dunia    tarehe 29 mei  1939 huko Roma;  alitangazwa Mwenye Heri na Baba Mtakatifu Yohani Paulo II huko Poznan-Poland tarehe 20 Juni 1983.

Alitangazwa Mtakatifu na Baba Mtakatifu Yohani Paulo II huko Roma – Italy  tarehe 18 Mei 2003.