Utume

Utume

Tangu mwanzo wa Shirika la “Waursula” lililoanzishwa na Mtakatifu Anjela Merici, waursula  wote duniani  ni walezi na walimu wa watoto na vijana.
Waursula kadiri ya karama yao wanafanya utume wa katekesi, kazi za Parokiani, vyama vya kitume, utume katika shule mbalimbali kama walimu wa shule za chekechea,

web 25

wa shule za msingi,

web 34

za ufundi

AP 22. issuna 3

na sekondari, ziwe za serikali au za binafsi.

Tanzania utume wa masista unaelekea zaidi katika kutoa  elimu ya kiroho na maadili kwa njia ya vyama vya kitume

kisawasawa1

katika Parokia, kwa njia ya kufundisha katekesi, maandalizi ya sakramenti na mara kwa mara kuwandaa watu wazima na wazee kuwa wakatekumeni.

Masista wanafanya kazi kwa watoto na vijana katika  nyumba za watoto yatima

dodoma askofu

na katika Hosteli zinazopokea  wanafunzi  wa shule za sekondari,  za ufundi na hata  wanafunzi wa  Vyuo Vikuu.

Katika nyumba ya watoto yatima – Dodoma – masista wanachukua nafasi ya wazazi (kama mama) wa watoto hayo yatima ambao  wazazi wao wamefariki kwa sababu ya ugonjwa wa ukimwi.

Na katika nyumba ya Leto-Rombo

web 28

masista wanachukua nafasi ya mama wa wale watoto wachanga  wakiwapa watoto wa miezi michache ule upendo ambao wameukosa kwa sababu mama zao wamefariki au wamewatupa.

web 37

Wapo masista wachache ambao wanafanya kazi ya unesi na ukunga hasa katika zahanati. Wapo masista ambao wanafanya kazi katika Hospitali ya Mt. Gaspari-Itigi, mmoja kama daktari ya watoto na mmoja kama nesi-mkunga.

DSCN1995

Katika kijiji cha Sukamahela masista wanatoa huduma kwa wakoma

sr Anitha 014

na Mkiwa masista wanawahudumia pia wazee walioachwa  peke yao na ambao wanahitaji chakula, nguo na hata nyumba.