Ripoti ya jubilei

MANENO MACHACHE
KUHUSU JUBILEI YA MIAKA 25 TANGU KUANZISHWA KWA MISIONI
YA MASISTA WA-URSULA WA MOYO WA YESU MTESWA
KANDA YA TANZANIA (1990 – 2015)
 

Jubilei ni Sherehe maalum za kuadhimisha tukio muhimu katika maisha ya mtu au Shirika hufanyika kila baada kipindi fulani yaani miaka 25, 50, 75 au 100 tangu kuanzishwa.

Uzinduzi wa jubilei hii ulianza rasmi kwa ufunguzi tarehe 25-9-2014. Uzinduzi huu ulitanguliwa na Misa Takatifu ambayo ilisomwa katika nyumba zetu zote za jumuiya ya wa-ursula Tanzania. Katika uzinduzi huu tulianza rasmi kusali sala ya jubilei iliyokuwa na madhumuni ya kumshukuru Mungu kwa maongozi yake na baraka nyingi alizotujalia katika Senta yetu ya Tanzania na Shirika kwa ujumla kwa kipindi cha miaka 25. Pia sala hii ilitenga kuwaombea wafadhili wa Shirika na hasa wale wa Senta Yetu na zaidi tuliomba neema ya miito kwa ajili ya Senta ya Tanzania na Shirika kwa ujumla. Ndani ya mwaka huu wa maandalizi ya jubilei Shirika lilijipanga kufanya mambo mbalimbali ili kuwasaidia masista kulifahamu shirika kwa undani zaidi na kuifahamu zaidi karama ya Shirika. Katika Mchakato huo, Shirika liliandaa Semina mbalimbali ambazo masista wote waliweza kushiriki kwa makundi. Katika semina hizi masista wote waliweza kuifahamu historia ya mama Mwanzilishi, Mt. Ursula, ya Shirika kwa ujumla na hasa karama ya Shirika.

Baada ya semina hizi kulikuwa na semina kwa ajili ya viongozi wa jumuiya zote za Senta ya Tanzania na katika Semina hii viongozi waliweza kujifunza na kupata mbinu mbalimbali za namna ya kuongoza jumuiya zao ( hivyo ilikuwa ni faida kubwa kwa viongozi)

Zaidi ya hayo ndani ya mwaka huu wa maandalizi ya Jubilei kulifanyika kazi mbalimbali za kuwakutanisha watoto na vijana ambao wanalelewa katika jumuiya zetu. Kwa mfano, watoto toka jumuiya ya Sukamahela walikwenda Dodoma na kukutana na watoto yatima wanaotunzwa na kulelewa katika jumuiya hii. Watoto kutoka Diagwa, Singida na Issuna walifika Mkiwa na kukutana na watoto wa Mkiwa. Watoto wa Mweka walikutana na watoto wa Leto-Rombo. Pia vijana wanaoishi katika hosteli zetu za Issuna, Mkiwa na Itigi walikutana Mkiwa. Lengo la kufanya hivi lilikuwa ni kuwakutanisha watoto na vijana hawa ili waweze kufahamiana na kuona kuwa wote wako chini ya uongozi wa masista wa-ursula. Na zaidi ya hayo kila walipokutana walipatiwa mafundisho mbalimbali,  maadili juu ya malezi na makuzi yao na maelezo juu ya Historia ya Mt. Ursula. Haya yote yalifanyika ndani ya mwaka mzima wa maandalizi kama Shukrani kwa Mungu kwa maongozi yake katika kipindi cha miaka 25.
Kilele cha jubilei hii kilifanyika tarehe 25-9-2015.
Siku tisa kabla ya kilele tulisali novena ya shukrani ili kumshukuru Mungu kwa mema na Maongozi yake aliyotutendea.
Katika kilele cha Jubilei hii kila jumuiya ilileta wawakilishi kutoka katika jumuiya zao. Pia tuliwaalika wageni mbalimbali wakiwemo mapadri na watawa.
Kabla ya Misa wageni waliona “presentation” ya historia ya Senta ya Tanzania; wageni walisifu kwa kuwaonesha picha halisi ya tangu mwanzo na mpaka kufikia kilele cha jubilei. Wengi walisema:  “Wanastahili kumpa Mungu sifa na utukufu kwani ni Yeye anayewaongoza”.
Baada ya “presentation” iliofanyila katika kanisa la “Moyo wa Yesu” yalikuwa maandamano kuelekea kanisa la Kristu Mfalme ampapo ilitayarishwa ukumbi kwa ajili ya Misa.

foto n. 1                     foto n. 2

Misa Takatifu ilikuwa nzuri na iliongozwa na P. Fransis Bartoloni kwa ruhusa ya Baba Askofu Edward Mapunda ambaye alikukwepo.

foto n. 3

Japo P. Fransis ni mwitaliano aliongoza Misa vizuri kwa kiswahili sahihi na hata mahubiri yake yalikuwa mazuri sana. Mahubiri  kwa undani alionesha lengo la masista kufika Tanzania na kuanza utume wao. Alisema lengo halikuwa tu kufanya utume au kuanzisha ukristo, bali lilikuwa kuingiza karama ya Masista wa-ursula kwa njia ya Shughuli mbalimbali walizozifanya na wanazozifanya mpaka sasa. Alisema pia masista walianza Misioni katika mazingira magumu sana kwani maeneo walioyoingia hayakuwa na maji, umeme na hata mawasiliano, lakini walipokea na kufanya yote kwa imani. Aliwasifu waanzilishi na utayari wao wa kuweza kukabiliana na mazingira hayo magumu ambapo uvumilivu wao ndio uliopelekea leo tunaadhimisha miaka 25 tangu kuanza Misioni ya Tanzania. Aliongeza pia kuwa masista tunapaswa kuwa tayari kufanya kazi popote kwa ajili ya ukombozi wa roho akirejeka maneno ya wosia ya Mt. Ursula.

Siku hiyo ya kilele cha Jubilei nyimbo za Misa na liturjia kwa ujumla ilikuwa na mpangilio mzuri. Nyimbo ziliimbwa vizuri, na kwa uchangamfu, hivyo watu walisikiliza kwa utulivu ujumbe uliokuwa ndani ya nyimbo hizo.  Misa waliimba masista kwa ustadi, pia kwa kilatini ambapo watu wengi hawaweza kuamini na ilikuwa tulivu na yenye kuvuta hisia ya watu
Furaha iliyofurika na kuonekana wazi kwa masista na kwa wageni wote.
Kulikuwa pia na Maandamano ya kupeleka Neno la Mungu na maandamano ya matoleo: yalikuwa mazuri sana.

foto n. 3a       foto 3 b

Kwa ujumla Misa ilikuwa inagusa miyoyo ya watu kwani kulikuwa na utulivu mkubwa.  Ulikuwa na maana hata uwepo wa watoto na vijana kutoka sehemu mbalimbali wanaolelewa na masista,

foto n. 4
Pia siku hiyo ya tarehe 25-9-2015, siku ya kilele cha jubilei, kulikuwa na uzinduzi wa pango (Groto) la Mama Ursula.

foto n. 5

Pango hili lilizinduliwa na kubarikiwa na Baba Askofu Edward Mapunda wa Jimbo katoliki  la Singida.

foto n. 6

Pango hili limejengwa kwa heshima ya Mtakatifu  Ursula kama kumbukumbu ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Misioni ya Tanzania na pia kama kumbukumbu ya miaka 150 kwa kuzaliwa kwake.
Mungu ametenda na anaendelea kutenda mengi kupitia masista wa-ursula.

Sifa na shukrani zimwendee yeye na Yote ni kwa Utukufu wake