Waursula ni akina nani

MUL 1

Shirika la Waursula wa Moyo wa Yesu Mteswa, ni moja la matawi mengi ya Familia ya Wa-Ursula iliyoanzishwa katika karne ya kumi na sita na Mtakatifu Anjela Merici.

Shirika hili, lilianzishwa na Mama Ursula Ledòchowska, aliyezaliwa tarehe 17 Aprili mwaka 1865 na alifariki huko Roma tarehe 29 Mei 1939. Alitangazwa Mtakatifu na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili tarehe 18 Mei 2003.

Mwaka  1920 Mama Ursula aliomba katika Makao Makuu ya Baba Mtakatifu ruhusa ya kubadilisha Konventi iliyojitegemea ya Mt.  Petersburg, pale ambapo yeye alikuwa Mama Mkubwa,  kuwa Shirika jipya la kitume la Waursula,  ambalo kwa mapenzi ya Kanisa lilipata jina la “Shirika la Waursula wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa”,

Tarehe 4 mwezi wa sita 1923 Katiba ya Shirika Jipya ilikubaliwa  na Makao Makuu ya Baba Mtakatifu   kwa majaribio  ndani ya muda  wa miaka saba.

Tarehe  21 Novemba 1930 Katiba ilikubaliwa  rasmi na kuwa katiba ya  kudumu