Roho ya shirika

 

s. cuoreMursula  kwa wito wake anajiunganisha kwa namna ya pekee na Fumbo la Mateso ya Kristo ambaye akitumwa na Baba, aliwapenda hivyo wanadamu hata kujitoa mwenyewe kama sadaka kwa njia ya  kifo  chake  msalabani. Kwa njia ya mateso yake wanadamu wote  washiriki kifo chake na ufufuko wake, ili waufikie uzima wa milele.  Masista wanajaribu kuitikia   neno la Kristu: “Ninaona kiu”  wakijitolea  mhanga  kikamilifu kwa upendo wa Moyo wa Yesu,  pasipo kiasi,  wakishirikiana kwa ajili ya wokovu wa wanadamu.

annuncia

 

Kielelezo  cha   maisha ya masista waursula  ni maneno ya  Bikira Maria aliyomjibu malaika: „Tazama  mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena” . Maneno haya ni „motto” wa  waursula wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa